Advertisements

Friday, February 5, 2016

SERIKALI YAELEZA KIFO CHA MWANAFUNZI MTANZANIA KILICHOTOKEA INDIA


Waziri Mahiga ametoa ufafanuzi huo leo bungeni, na kuthibitisha ni kweli wanafunzi hao wamefanyiwa vitendo hivyo, ambavyo watanzania walikuwa wanavisikia bila kuwa na taarifa rasmi.
“Wananchi wa India walichoma gari lake, na punde kidogo gari lingine lilifuata likiwa na wanafunzi wanne watanzania, mmoja msichana na watatu wavulana, walilisimamisha lile gari na kuwavuta wale wanafunzi nje, na wakamchukua yule msichana na kumvua nguo na kuanza kumtembeza barabarani uchi, wale wavulana walipigwa na gari lao lilichomwa, katika gari lile kulikuwa na simu zao na documents mbali mbali nazo ziliteketea”, alisema waziri Mahiga.

Waziri Mahiga aliendelea kwa kusema kuwa baada ya hapo askari wa India walifika lakini hawakuonyesha ushirikiano wa kutosha, lakini wanafunzi hao walipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ya majeraha waliyokuwa nayo, lakini walilazimika kuondoka mapema kwa kuwa hawakuwa na pesa.

“Baada ya hapo ubalozi wetu wa India uliandika dokezo la kidiplomasia kwa serikali ya India, ikilaani kitendo hicho na kuitaka serikali ya india ichukue hatua za kisheria na haraka katika kupeleleza kufuatia matukio hayo, na waziri wa mambo ya nchi za nje wa India, alitoa taarifa rasmi kule New Delhi,kwanza kuomba radhi kwa Tanzania na watanzania walioko India kwa kitendo hicho kilichotokea, akaagiza serikali yake ichukue hatua za kisheria na kupeleleza na kukamata wale waliohusika, na wote sasa wamekamatwa na wamepelekwa mahakamani”, alisema Waziri Mahiga.

Pamoja na Hayo Waziri Mahiga alisema serikali India iliagiza kwamba wanafunzi wa Tanzania wapewe ulinzi maalum kule wanakoishi na kusindikizwa pale wanapokwenda masomoni au madarasani , na tatu serikali ya India ilimtaka balozi wetu afuatane na maafisa waandammizi wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya India mjini Bangalow, ili kukutana na wanafunzi wa Tanzania na wengine wa Afrika, na kuweka mahusiano mazuri kati ya wananfunzi na wenyeji katika mji huo.

Pia Waziri Mahiga alitoa taarifa rasmi juu ya kifo cha mwanafunzi mwingine Mtanzania nchini humo, na kusema mwanafunzi huyo hakufariki kwenye tukio hilo la uvamizi, bali alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha kifo chake.

“Nilielezwa kwamba kuna mwanafunzi mmoja ambaye amefariki karibu na maeneo hayo hayo , taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha wakadhani kifo hicho kilitokana na tukio hilo la kuvamiwa wanafunzi wetu, lakini si kweli, mwanafunzi huyo mtanzania alikuwa anaendesha piki piki bila kofia, akaenda kugonga nguzo ya taa na kufariki pale pale, ubalozi wetu unashughulikia mazishi na mwili wake utarudishwa Tanzania mapema iwezekanavyo.

Tukio hilo limeingia siku ya tatu sasa tangu kutokea kwake nchini India, ambapo kumeibuka hisia tofauti tofauti miongoni mwa watanzania, na kuwatia hofu wanafunzi wanaosoma nchini humo.

No comments: