Advertisements

Monday, October 5, 2015

EMMANUEL MBASHA NI NANI ALIKUROGA???


Ndoa na mapenzi ni mambo ambayo mara nyingi huwa hayaingiliwi,yametawaliwa na msemo kuwa'mapenzi ni wawili tu akiongezeka wa tatu ni mchawi',lakini pia huwa inapobidi watu wanaingilia hasa pale wahusika au mhusika mmoja anapovuka mstari mwekundu,
Hakuna asiyejua sakata la mbasha na mkewe flora,huyu jamaa alituhumiwa kumbaka shemeji yake,mmoja wa shahidi muhimu upande wa mashtaka alikuwa mkewe flora,ina maana flora alitaka mumewe aozee jela,na kweli wakati kesi ikiendelea flora alienda mahakamani na kutoa ushahidi wa kumkandamiza mumewe ili afungwe,
Mungu mkubwa hukumu ilipotoka mbasha kashinda kesi na sasa yupo huru,kilichoshangaza umma wa watanzania ni kauli ya mbasha kuwa bado anampenda sana mkewe flora na yupo tayari kuendelea kuishi nae,najiuliza kwa vitendo vyote alivyotendewa na huyo mwanamke bado anampendea nini?Huyu jamaa alirogwa?
Amerukwa na akili? Unampendaje mwanamke aliyetaka uozee jela? Watu wa karibu na mbasha msaidieni huyu jamaaa maana anakoelekea ni kutafuta kifo,msimcheke pls msaidieni tu.

Source:Jamii Forums...By The Counseller

2 comments:

Unknown said...

Mapenzi ya kikolea, huwa yanasamehe.

Anonymous said...

Kusamehe kupo lakini ajiulize je, mkewe bado anampenda au alikuwa ameshamchosha kwa hiyo alikuwa anatafuta njia ya kuachana nae kabisa. Maana km angefungwa kwa kubaka, huyo mke asingemrudia mbakaji! Kuwa makini wewe mwanaume. Kwa maombi uliomwomba Muumba wako, ujitambue km mke bado anakuhitaji au atakutafutia njia nyingine tena ya kukundoa ktk maisha yake. si wa kwanza kusamehe bali wako hata wanawake wengi yamewakuta mwishowe mambo yankuwa mabaya zaidi au mazuri. Inategemea na muhusika atajirudi kiasi gani!