Advertisements

Sunday, October 4, 2015

TANZIA


MCH. CHRISTOPHER MTIKILA AFARIKI KWA AJALI YA GARI MKOANI PWANI
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
RPC Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao wamejeruhiwa.
Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. 
Hili ndilo gari alilopata nalo ajali merehemu Mch. Christopher Mtikila

ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAAARIFA ZAIDI

CHANZO: TBC TV

2 comments:

Anonymous said...

Poleni sana familia nzima pamoja na watanzania wenzangu huyu mzee anafahamika kwa miaka mingi akiwa anagombea haki za watanzania mungu amuweke mahali pema peponi

Anonymous said...

Mchungaji tutakukumbuka sana kwa mchango wako mkubwa katika siasa za nchi yetu. Kwa hakika tukukosa sana. Hata hivyo yote hii ni kazi yake Mwenyezi Mungu ambayo haina makosa kwani ndiye mtoaji na pia ndiye mtwaaji. Mchungaji Mtikila R.I.P.