Advertisements

Wednesday, September 2, 2015

LOWASSA AENDELEA "KUTISHA" MAELFU WAFURIKA KUMSIKILIZA HUKO RUVUMA

MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na Othman Michuzi)

5 comments:

Daniel said...

Lowassa hakamatiki. Kila njama watakayotumia haiwezi kufaa. Watu wamechoka na CCM

Anonymous said...

AMA KWA HAKIKA ANAENDELEA KUTISHA KWA UFISADI.

Anonymous said...

Lowasa atimshe na nani hao watu katika picha hawakaribii hata robo ya umati anaoukusanya magufuli. Hivyo vijihela vyake vichafu bado vinaendelea kuvinunua vichwa vya habari vya baadhi ya vigazeti nchini.

Anonymous said...

Ni vyema waTanzania na hasa utawala huu wa kiimla ukubaliane kuwa mabadiliko yapo na wasinunue sana wanasiasa ili kudhoofisha pale panapoonekana panafaa. Hizo fedha wanazotoa kwa wanasiasa nankuwapa siri za kutoa hadharani kuwakodishia hoteli kwa gharama kubwa ni fedha ambazo zingewasaidia wananchi kuboresha shule na miundo mbinu mibovu. Tusiendeleze aina hi ya ufisadi. Na tuelewe Ufisadi sio kuhodhi fedha wala nyumba tu hata kutokuwajibika ipasavyo ukiwa kiongozi ni aina mojawapo ya ufisadi na ni mbaya sana ndio ulokotufikisha tuliko.

Anonymous said...

CCM mwaka huu mmekwisha.