Advertisements

Tuesday, September 1, 2015

DK.SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
 
Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroad Slaa amesema leo kuwa amejiondoa kwenye siasa na hatajiunga na chama kingine chochote cha siasa ila ataendelea kuwatumikia Watanzania kwa namna yoyote.
Dk Slaa amesema alichukua uamuzi huo tangu Julai mwaka huu baada ya kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea mgombea wa urais kupitia Chadema chini ya mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa.
Dk. Slaa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, amekiri kushiriki vikao kujadili ujio wa waziri mkuu huyo wa zamani lakini alishangazwa na viongozi waandamizi wa chama chake kuharakisha kumpokeea pasipo kutimiza masharti aliyopendekeza.
“Sina tabia ya kuyumbishwa….sina chuki na mtu yoyote lakini sipendi siasa za udanganyifu na propaganda,” amesema Dk. Slaa na kusema ameachana na siasa tangu 28 Julai, 2015 baada ya kuona misingi ya chama alichoshiriki kukijenga imepotoshwa.
Sharti la kwanza ambalo Dk. Slaa alitaka lizingatiwe ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya serikali ya CCM kujisafisha kwenye tuhuma ya kashfa ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa kama Waziri Mkuu.
Aidha, Slaa alitaka ajue Lowassa ataongeza thamani gani ndani ya Chadema, ikiwa ni pamoja na viongozi watakaojiunga toka chama tawala.
Baada ya Lowassa kutokidhi vigezo tajwa, huku akiwataja viongozi waliojiunga Chadema wakitokea CCM wakiwa ni “mizigo” ndani ya chama tawala, amejiweka kando na Chadema.
DK Slaa ametumia takribani saa mbili kueleza msimamo wake na matatizo anayoyaona kwa Lowassa na waziri mkuu mstaafu ambaye naye amejiunga na upinzani, Frederick Sumaye kuwa hawafai na si watu safi.

22 comments:

Anonymous said...

Ni wazo zuri tu mheshimiwa Dr Slaa. Ukaamua kumpumzika kisiasa ukakaa na mama masehap wako nini shidaa waache wenye nguvu waendelee. Tunakutakia amani na maisha mapya.

Anonymous said...

Kwaheli Dr Slaa
Lakini tutasikia mengi naona sasa utakuwa Dili ya kuichafua ukawa Toka ccm
Ikumbukwe wengi wamehama ccm tena maziri wakuu wastaafu wenyeviti wa mikoa
Lakini ccm ipo
Hata wewe kuhama chadema
Chadema haitakufa
People's power

Anonymous said...

Nampongeza Dr.Slaa hasa kwa kuitumia demokrasia na haki yake ya msingi ya kuongea na kutoa msimamo wake.
Ni ishara nzuri na ya uungwana kukubali kutokubaliana.
Hata mzee kingunge nae pia aliona ukiukwaji wa utaratibu katika chama chake alicho kitengeneza kwa maisha yake yote.
Mchango wako kwa mageuzi Tanzania na kwa chadema utadumu milele. Nasikitika umejitoa hivi sasa wakati harakati za msingi zinaendelea, but ni haki yako ya msingi kufanya maamuzi ya aina yoyote kama mtu binafsi.
Harakati za ukombozi wa Tanzania nadhani zinaendelea vizuri tu, ukombozi is beyond one individual it a nation effort. Lowassa, Sumaye, Mbowe, Maalim Seif na vinara wengine nadhani ni figures tu ambazo zipo kwa kipindi hiki kufanikisha leng kuu la ukombozi. Sooner or later watapita na harakati zitaendelea.
Labda sote turejee hotuba na sala aloifanya mchungaji Kakobe siku ya kumtangaza Lowassa, ni ujumbe tosha. Hakuna mwanadamu alie msafi, tuvumiliane na ku focus kwenye lengo kuu. Kulikomboa Taifa kunahitaji bold stand.
Aluta Kantinua

Anonymous said...

Dr. Slaa. Karibu tena kwenye utaifa. Huna wa kumlaumu kwani mchakato mzima ulijikita ndani ni sehemu ndogo sana ilikushinda kwa kutokubali uzalendo. Ukitambua wazi kabisa siasa ndivyo ilivyo
Na uchambuzi uliofanyika tangu mwezi March unaujua kabisa alimia ngapi zilikuangukia hivyo hukuwa na sababu kususa umlikokuwa umefikia. Kama una maamuzi ya kujipumzisha kisiasa basi vyema ukarejea uchungaji na huko nako kuna kama haya haya si uliondoka huko nahuku nako sheedaah!! Umechelewa gear libwa ishawekwa na wako angani utawapata wapi. Kweli unaitakia Tanzania na watu wake maendeleo au mageuzi??!!

Anonymous said...

Hongera kwa kusimamamia kile unachokiamini -Maadali. Tanzania bila kuwa na viongozi, watumishi wa uma na jamii kwa ujumla inayofuata maadili tusitegemee mabadiliko yoyote regardless ya nani au chama gani kitashinda coming October. 2015

Anonymous said...

Pumzika Slaa. Hata kwenye ile safari za kotoka Misri kwenda Promise Land wengi walipumzika na hawakufika, Wengi walikufa njiani na wengien kubakia kulalama kwa Mungu. Waliofika Pomise Land ni wale waliokuwa na imani kuwa watafika.

Anonymous said...

Siasa za kipuuzi hizi huyu Jamaa hana washauri wa kumwambia Hana mvuto wa kuufanya UKAWA kuchukua dola. Hivyo ingekuwa busara Kunyamaza mpaka Baada ya uchaguzi. Kauli hizi zinaonyesha jinsi ulivyokuwa unauota urais mpaka kukosa usingizi. Kuna watu ndani ya CCM walikatwa wakasema wananyamaza mpaka Baada ya uchaguzi, haya maneno ni kukipaka kitumbua cha mwenzio mchanga

Anonymous said...

Ana haki kikatiba ku express his opinion. Na sio kila mtu ni coward. .

Anonymous said...

Toa ushahidi wa Dr.kutumiwa na CCM.

Anonymous said...

Nonsense! Mafisadi ndiyo wana mvuto?

Anonymous said...

Kwa kweli hongera sana sana dk slaa umeonyesha jinsi gani ulivyokuwa na msimamo wa kweli. Tunajua jinsi gani watu walivyokuwa wakikulazimisha kula matapishi yako . Tunajua wewe ni mwanamageuzi wa kweli isipokuwa matapeli ya kisiasa yanajaribu kukutengenezea zwengwe ili uonekane wewe ndio mwenye matatizo. Watanzania wanajua licha ya maneno mengi yanayosemwa ya dharau dhidi yako kwenye vikao vyao vya chama, kwenye mikutano yao hadhara na mitandao ya jamii chadema na ukawa kwa ujumla pamoja na wafuasi wao wanajua wamepata pigo na sasa wanaweweseka wamefanya kosa ambalo watalijutia maishani mwao yote. Isipokuwa hutawatendea mema watanzania kuachana na siasa na kuwaacha matapeli na utapeli ulioukataa wakitafuta kila ujanja wa kuwalahi wanachi ili waitafune hii nchi . Tunajua wewe dk slaa ni mpiganaji wa kweli wa kiroho na vitendo kwa hivyo watanzania tunakuomba uungane na nguvu sahihi ya kupigana na huo utapeli, udanganyifu, uwongo, upotoshaji, brain washing propanda za ukawa kwa watanzania na kwa mtu yeyote yule mwenye kuitakia mema Tanzania na watanzania basi hakuna nguvu sahii na muokozi wa watanzania na taifa Lao na mali zao na maisha yao kama Maghufuli.

Anonymous said...

Kwaaaaa kwiii tiiiii ,DR SLAH shikamoo ,umejua kawafyeka makalio hawa chadomo watabaki wanakusema ovyo lakini kumoli roho zina wauma umewaarishia utosini na bado endeleeni kubwabwaja kwasababu huwa ampendi mtu kuwaambia ukweli mkiambiwa ukweli na mtu mmesha muona adui na viongozi wenu nawambia wakiendelea kumtibua huyu mzee mtajutraa mzee anakila kitu chenu ajali huyu atamwaga kila kitu mezani mpaka sasa hivi CCM imeshashinda .ngoja ninywe pombe yangu hapa ya wanzunki kichwa itulie .

Anonymous said...

Mh. Sana Dr Slaa. Tunakushukuru waTanzania. Hii yote ni njama na juhudi za Chama Tawala baada ya kukufuata saana na mkeo baada ya hili jambo kutokea. Huu ni mkono wa CCM kutaka kupunguza nguvu ya mafuriko. Ila tunasema hiyo fedha uliyochukua toka CHAma Hii na kukuandalia huo mkutano hHoteli kubwa kiwango hicho hutadumu nayo na mapambano yanaendelea leo ushindi ukipatikana utahama nchi? Mbinu za magoli ya mkono umekubali kuuyaunga mkono tena ndani ya penalti. Huwatakii mema waTanzania na hukuwa mwanasiasa mkweli.. Mungu bariki mabadiliko. Fedha si ushachukua..

Anonymous said...

Keep it up !! Mzee wangu, wewe ndio kweli Mzalendo wa kweli mwenye uchungu wa kweli kwa nchi Yako na wananchi wote wa Tanzania!iii nimekupenda sana Dr Slaa Kwani mie pia na uchungu wa kweli kwa nchi yetu inavyoibiwa na sisi tunaangalia tu Kama tumeshakata tamaa na maisha. Lakini tuongee u kweli Watanzania wenzangu, kweli katika watu wootee wanaoweza kuchaguliwa kuongoza nchi kweli inawaingia akilini kumshabikia Lowasa Lowasa!! Of all the people!! Mwizi mkubwa! Fisadi Mkuu!! Kweli mmekata tamaa ya maisha katika nchi yenu!!! Huyo ni Magamba wa Ccm 100% wote mnajua! Atakuwa na jipya lipi???!! Amekaaa madarakani Miaka mingapi hakuwahi kuwaletea maendeleo Leo anawadanya kama watoto wadogo kweli mnamwamini!!!?? Eeeh Mungu tusaidie sisi Watanzania tunaokuwa Kama tumelaaniwa!! Ni Mara Elfu Mia Moja mkimchagua huyo wanayemwita Magufuli kuliko huyo Mchafu ambayee hakuna aina yoyote ya sabuni itakayoweza kumsafisha!! MUNGU IBARIKI TANZANIA ! MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Anonymous said...

Dr. Slaa angekuwa na mshauri wa siasa asingeongea upuuzi aliouongea kwa muda wa masaa mwaili. Ile kitu watanzania wanataka ni mabadiliko. Hata kama ni kupigia kura jiwe, ni afadhali kukipigia kura ccm. Watu wote walioko ccm ni corrupt wa siasa, wa rasilimali za nchi n.k. sielewi inakuwaje Dr. Slaa ameshindwa kuangalia pande mbili za shilingi (two sides of the coin). Angeeleza pesa za escrow ziko wapi, akalinganisha epa, na richmond, na wale twiga waliopanda ndege kwenda Swissland tungemwelewa kidogo. Dr. Slaa amekuwa traitor wa ile kitu anachokiamini. Kama alikuwa anataka kuuondoa mfumo wa utawala ulioko mafarakani, alitakiwa ahishiriane na wenzake wa ukawa mpaka kieleweke. Anaposema anaachana na siasa halafu anashambulia upande mmoja crebility ya kile anachoamini na kukisema kinabaki kuwa ni swali (very much questionable). Binafsi nilikuwa namheshimu sana dr. Slaa lakini hii ya press conference leo, nimejua ameishiwa sera! He needs a break. Kwanza ajue kwa chadema kina sera, kina katibu mkuu mwenyekiti na halmashauri kuu. Wale wote wanaochukua dhamana ya kutawala kuwa viongozi wa serikali watakuwa responsible kwa chama na sera zake. Chadema inataka kuleta uhuru wa mawazo ya kila mtanzania wa kudhaminiwa kama binadamu, uwazi na ukweli, usimamizi wa rasilimali za tanzania kwa ajili ya watanzania. Sasa wewe slaa unavyorudi nyuma kwenye haya mapambano, hata Mungu unayemwamini atakushangaa sana. Mungu Akupe pumziko zuri katika maisha yako nje ya siada. Sisi tu naendelea na mabadiliko. MABADILIKO UKAWA,ABADILIKO CHADEMA, MABADILIKO NCCR, MABADILIKO CUF MABADILIKO NLD, MABADILIKO NI LOWASSA. SISI WATANZANIA ZAIDI YA ASILIMIA 90 KUANZIA ULIPO MALIZA PRESS CONFERENCE
YAKO HATULALI MPAKA KIELEWEKE. BYE BYE SLAA. TUNASUBIRI TANZANIA MPYA BILA YA CCM YAWEZEKANA. EEH MUNGU TULE TEE TANZANIA MPYA ISIYOKUWA NA CCM ISIYOKUWA NA VIONGOZI WA MAJIVUNO KAMA VIONGOZI WA CCM..viongozi wenye matusi kama wa ccm

Anonymous said...

Na ahame bibi
Cha ajabu kitu gani
Wamehama mawaziri wakuu wastaafu ccm na mawaziri wenyeviti wa mikoa , na wabunge kuhamia ukawa lakini ccm si ipo
Sembuse yeye kwanza alikuwa zigo kwetu siasa za kitanzania ziende kibongo na ndiyo tulivofanya kumchagua lowassa

Anonymous said...

No sense, unauiita upuuzi kwa kuwa hakuongea ulichokuwa unatarajia.Dr. ameongelea facts, mjibu kwa hoja kama alichokuwa anaongea ni kweli au la.Nilitegemea Lowasa kukanusha maneno hayo mbele ya uma.

Anonymous said...

Ulikuwa na ulazima gani wa ku comment. Sioni ulichoandika.

Anonymous said...

Toa ushahidi wa kuwa CCM inahusika na maelezo aliyoyatoa Dr.Si lazima kubeba na kuamini taarifa ya Slaa kwakuwa si wote wanauwezo wa kuona tofauti kati ya chuya na mpunga.Tukutane.baada ya October baada ya Magufuli kuchukua nchi.Wex2 nenda na mafuriko..

Anonymous said...

No sense, awaache wenye nguvu ya ufisadi waendelee bila kuambiwa.Tafakari zaidi.

Anonymous said...

Bakia na unachotaka ww nani akubadili kama huwezi soma ukaelewa..

Anonymous said...

Hujajua uliko na umekalia kuti kavu litapoporomoka usishangae. Endelea kutafakari wakati treni ishaondoka.