Advertisements

Saturday, August 1, 2015

Ukweli kuhusu Dr. Slaa by A.N Chilongola (LLM)

Taharuki imetanda juu ya wapi alipo Katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa. kila mtu anazungumza lake kwa kadri anavyoelewa. wengine wakisema yupo kwenye maandalizi ya vikao vya kamati kuu na wengine wakisema amejificha kwa sababu hakubaliani na maamuzi ya kumleta EL kwenye chama.

Mimi kama kada wa chadema wa muda mrefu na mwanasheria mzoefu nimefanya utafiti na nimejiridhisha bila shaka yoyote kuwa hali si shwari ndani ya chadema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa kuonesha kuwa hakuna tatizo.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kuwa Dr.Wilbroad Slaa hakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu ya Kumleta EL na kumpa nafasi ya kugombea Urais bila kufanya utafiti wa kutosha. Slaa anadai kuwa maamuzi haya ni ya haraka mno na chama kilitakiwa kijitafakari zaidi kabla ya kumpa ridhaa ya kugombea Urais.

Ikumbukwe siku ya jumapili tar.26 wakati UKAWA wamefanya kikao cha mwisho na EL Dr.Slaa alikuwepo na baada ya hapo akapotea kabisa na hajaonekana hadharani hadi leo.


Ukweli ni kwamba ndani ya kikao kile chs jumapili Slaa alionesha msimamo wake juu ya EL na kudai kuwa watanzania hawatatuelewa wakituona tukipita kumsafisha mtu yuleyule tuliyemchafua awali.

Hivyo Slaa akatoa masharti mawili makubwa. La kwanza ni EL aitishe Press na ajisafishe mwenyewe kabla hajatangaza kuja UKAWA. Aruhusu waandishi wamuulize maswali yote kuhusu Richmond na kashfa nyingine ikiwemo umiliki wa jengo la Ubalozi wa S.Africa na EL ajibu hoja zote kwa maelezo ya kueleweka. Sharti la pili la Slaa ni kuwa EL asupewe nafasi ya kugombea urais kwa sasa kwani ni ngumu kupima dhamir yake kama ni ya kweli. Slaa akapendekeza EL aje CHADEMA na aisaidie UKAWA kuchukua dola bila kugombea Urais.

Lakini Mbowe akampinga sana Slaa na akasema Katibu mkuu hawezi kuweka "ultimutum" ya EL kujiunga na chadema. Mbowe akapuuza mawazo ya Slaa na akaagiza mchakato wa kumpokea uanze mara moja na kesho yake Mbatia akaambiwa atoe tamko la kumkaribisha EL UKAWA.

Hali hii ilimfanya Slaa kujihisi mnyonge na aliyepuuzwa. akahisi hathaminiki ndani ya chama licha ya mchango mkubwa alioutoa kukijenga chadema. jambo la ajabu Mbowe alipopelekewa taarifa hizo alijibu kwa kejeli kuwa liwalo na liwe. yani yuko tayari kumpoteza Slaa na kumkumbatia EL.

Haikujulikana wazi Mbowe ana maslahi gani katika hili la EL na kwanini aamue kuwa na msimamo mkali hivyo wa kumtetea EL.

Inadaiwa tangu jumapili Slaa alipoachana na viongozi wenzie wa UKAWA hadi sasa yupo ndani hajatoka na hakuna mgeni anayeruhusiwa kumuona. Anautumia muda huu kusali na kushauriana na marafiki zake kwa njia ya simu (wengi ni maaskofu) juu ya nini afanye katika kipindi hiki.

Wengi wamemshauri aachane na siasa na ajiuzulu nafasi yake ya SG ndani ya chadema wazo ambalo limeungwa mkono na mkewe Josephine na baadhi ya watu wenye misimamo mikali.

Baada ya ushauri huu mkewe wa Slaa ameonekana kufurahia na ameanza kuelezea kwenye mitandao ya kijamii. Jsna kupitia kundi la Nyakahoja la whatsapp Josephine alisema mumewe ameteseka sana na chama hiki na amekitoa mbali sana. Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Anasema ni afadhali Mbowe angesikiliza ushauri wa Slaa wa EL kujisafisha kwanza kabla hajaja chadema maana kuja bila kujisafisha ni kuwaweka viongozi wote wa chadema kwenye mtego.

Madai ya Mbowe kupewa fedha na EL. Yapo madai kuwa Mbowe amehongwa sh. bil 12 ili kumpokea EL. Fedha hizi ameziweka kwenye akaunti yake binafsi na amewawia kidogo wale aliowaona wanaweza kumchallenge. baadhi ya watu waliopata mgao ni wajumbe wa kamati kuu ili kuwaziba mdomo. na si wajumbe wote bali wale wachache viherehere. baadhi yao ni Godbless Lema (anadaiwa kupokea milioni 120), Peter Msigwa (mil 135), Tundu Lissu (mil 180), Salum Mwalimu (Mil 180).

Pesa hizi ndizo zinazodaiwa kuwafumba macho kamati kuu na kuamua kumpitisha EL bila kufikiri mara mbili. Kitu cha ajabu kamati kuu imefunga dirisha la kuchukua fomu na kusema eti kamati kuu inamuunga mkono Lowassa tu.

Huu ni ujinga ambao hata CCM haiwezi kuufanya. Kamati kuu inatakiwa kuwa neutral. kamati kuu haitakiwi kuwa na mgombea. kamati kuu haitakiwi kuzuia watu kuchuku fomu. acha wachukue wengi kadri iwezekanavyo halafu wachujwe abaki mmoja.

Kama EL anajiamini yeye ni bora zaidi na ana nguvu zaidi kwanini anaitumia kamati kuu kuzuia watu wasichukue fomu? Siku chache zilizopita watu walilalamikia kamati kuu ya CCM kuwa ilikua na mgombea wake mbona hawaoni hili la kamati kuu ya chadema?

Ikiwa madai haya ya kuhongwa kamati kuu ni ya kweli basi chadema inaelekea ukingoni katika siasa za nchi hii. jambo la ajabu viongozi wanaodaiwa kuhongwa akiwemo Mbowe hawajakanusha habari hizi. halafu wanatuma ujumbe kw Slaa eti wakamsihi asiondoke. wajumbe wote waliotumwa wakaishia getini na hawakufunguliwa mlango. mlitegemea mfunguliwe mlango wakati kuna madai mmehongwa na hamjakanusha? kanusheni kwanza ndio muende kumuona Slaa. Au mnataka mkamhonge na yeye? Kama msipokanusha habari hizo mkienda mtafungiwa tena nje maana nyumbani kwa Slaa hakitaingia chochote kilicho kichafu.

Response ya Chadema. ni kama vile hawajali yanayoendelea. na bahati mbaya zaidi vijana wa chadema wameanzisha movement ya kumtukana Josephine kuwa yeye ndio anamponza mumewe. kwenye mtandao wa jamiiforums, facebook ma magroup ya whatsapp wanamtukana sana.

kwenye group moja la wabunge wa chadema wameanzisha movement iitwayo "Josephine Bring Back our Dr". wengine wanamwita mwanamke mpumbavu, wengine wanasema ana hasira ya kukosa ufirst lady, lakini wengine wamefika mbali na kudai anatumiwa na TISS na CCM.

Kimsingi madai yote hapo juu hayana mashiko. Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini. anachofanya ni kutetea haki ya mumewe. haki ya kuthaminiwa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kutoa mawazo yake na kusikilizwa.

Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa fedha na hawajakanusha habari hizo, halafu ukimtetea mumeo unaambiwa unatumika na TISS. this is ridiculous.

Hakuna cha TISS wala CCM mchawi wa chadema ni chadema wenyewe na mchawi wa ukawa ni chadema. Hizi porojo za TISS ni mbinu inayotumika ili Slaa akiamua kutangaza msimamo wake ionekane anatumiwa na CCM. Chadema acheni siasa za kitoto. hivi Slaa aliyepigania chadema zaidi ya miaka 20 akitoa sadaka maisha yake kwenu ndio wa kutumika na TISS leo aache kutumika huyo EL aliyekuja jana? this is very interesting. chadema kitaingia katika rekodi za dunia za kuwa chama cha kwanza kumtilia shaka mwanachama wake wa miaka 20 na kumuamini mwanachama wa siku moja.

Nini kifanyike? Jambo linaloweza kufanyika na kusaidia kuiokoa chadema na UKAWA kwa ujumla ni mediation. zitafutwe mbinu nzuri za kukutana na Slaa na kuongea nae. aeleze yanayomhusu na chama kioneshe concern ya kuyatatua.

pia kwa kuwa Josephine anaonekana kuwa na nguvu kubwa sana kwa Slaa hivi sasa ni bora Watafutwe wanawake wenye heshima ndani ya chama wakaongee nae. kwa mfano Mama Regina Lowassa, mama Ntagazwa na mama Mbatia waende kumuona mwanamke mwenzao waongee nae. hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama maana tangu juzi anatukanwa mitandaoni akidaiwa ndiye anayemzuia Slaa.

Ni vizuri mambo haya yafanyike mapema maana taarifa zilizopo ni kuwa kufikia wiki ijayo kama chama kitakua hakijatoa msimamo kuhusu Slaa basi yeye atatangaza msimamo wake wa kujiuzulu wadhifa wake chadema na kuamua kuachana na siasa kabisa. kisa wataondoka nchini yeye na familia yake kwenda Italia ambapo ataishi huko kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini na kumalizia maisha yake Karatu. mipango ya Slaa kwenda kuishi Italia kwa miaka mitano inaratibiwa na shirika mija la kiroho la kanisa katoliki na maandalizi yanaendelea vizuri.

Hivyo basi ni vema kazi hii ikafanywa mapema na kwa umakini ili tusivuruge kazi yote ya kuijenga Ukawa na kuujenga upinzani nchini. ukweli ni kuwa Slaa akiamua kujiuzulu siasa za upinzani zitapoteza uelekeo na tutashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kuanzia udiwani, ubunge hata urais. maana yake ni kuwa kazi yote iliyofanyika kuujenga upinzani inabomolewa siku moja na kuifanya CCM izidi kushamiri. na ikiwa Slaa ataondoka itachukua miska zaidi ya 100 kupata upinzani mwingine wenye nguvu kama huu. hivyo basi juhudi za haraka zinatakiwa.

Mwandishi wa makala haya ni ndugu A.N Chilongola, mwanachama wa chadema na mkurugenzi wa kampuni ya uwakili ya Chilongola &Advocates iliyopo Mabibo Dar.anchilongola@gmail.com

10 comments:

Anonymous said...

Mbowe,tundu lisu, lema, peter msigwa, mbatia, seleman athuman na kamati ya kuu ya chadema shame on you!!!!! Njaa inawafanya mnanunuliwa na kuiuza demokrasia ya nchi yetu. Watanzania na wanachadema waogopeni hawa ukawa feki na lowasa kama ukoma. Toka chama kikawa na mgombea mmoja wa kuchukua fomu, wapi demokrasia ya kweli?!!!! Hivyo vijisenti ndio mnataka kuiangamiza nchi yetu kwa hiyo traitor. Watanzania sio wapumbavu kama nyinyi na ataanguka vibaya sana kama atafika katika uchaguzi maana takururu tayari wameshaanza kazi yao. Mahakama inamsubiri in few weeks

Anonymous said...

Dr.Slaa na wale wanaopinga ujio wa Lowasa wanatakiwa wasome alama za nyakati kwa manufaa ya Upinzani,wananchi na Taifa kwa ujumla.Ni kweli Dr.Slaa alikuwa anatarajia kuwa yeye atagombea urais kupitia UKAWA lakini kwa hali ya siasa ilivyogeuka ghafla nchini ni vyema Chadema na UKAWA wakatumia hii opportunity ya ujio wa Lowasa kushinda ubunge kwa wingi na hata uraisi ili kuleta BALANCE ya kisiasa nchini.
Lakini pia Dr.Slaa alishawahi kugombea uraisi mwaka 2010 na matunda yake yalionekana kwa hiyo ni wakati wa kuwapisha wengine wagombee na huo ndiyo upevu wa siasa na siyo kuendelea kug'ag'ania kugombea na kukosa yote.

Anonymous said...

PAMOJA NA KUDAI KUWA UMEFANYA UTAFITI MAMBO MENGI UNAYOYAELEZA HAPA NI "SPECULATIONS" KWA KIFUPI HUU SIO UTAFITI BALI NI MAONI YAKO NA ILI KUTAFUTA IONEKANE UNACHOANDIKA KINA SHABIHIANA NA UKWELI, UMEJARIBU KUOAINISHA KWA KUWEKA VIONJO VYENYE UKWELI. HATA HIVYO HONGERA KWA KUWA UMEFANIKIWA KUFIKISHA UJUMBE WA KILE UNACHODHANIA KIMETENDEKA, NA PIA UMEWEZA KUFIKISHA MALALAMIKO YAKO BILA KUPAAZA SAUTI (USING A REPORTING SPEECH)

Anonymous said...

Ni masikitiko makubwa kwa Chadema. Tumempokea FISADI ambaye amekwisha infect Chadema leadership yote na ugonjwa wa UFISADI. To bribe Mbowe with Tshs.12 Billions is a very serious political corruption scandal in the history of Chadema; and frankly speaking, it is pathetic and unacceptable. TAKUKURU have to look into this. Watanzania wenzangu, try to imagine, jee? serikali ya Chadema itakuwaje? Kweli nyinyi viongozi wapiga debe wa Lowasa mmetufanyia wanachama wa Chadema haki? You have betrayed us, and both of you need to be sacked. No wonder why CCM walimtupa kapuni huyu ndugu Lowasa. No reasons to vote for him, because Lowasa was corrupt then, and will continue to corrupt our country while he is at Chadema.

Anonymous said...

Yaani namuoenea huruma mzee wetu Slaa. Kazi alioifanya ya kuijenga chadema kwa zaidi ya miaka ishirini inaishia mikononi mwa wajanja na yeye kuonekana si lolote kwa kweli inasikitisha kiasi mzee wetu ajifungie milango . Yaani sawa na mtu kuwa unajenga nyumba kwa miaka 20 karibu ya kuhamia anakuja mtu anakwambia mimi ndie mwenye haki ya kuhamia na wale watu waliokuwa wanakusaidia kuijenga hiyo nyumba wanakuwa pamoja na mwenye kuchukua haki yako kwa kweli huo ni usaliti wa hali ya juu. Dr slaa Kutokana na cheo alichofikia katika taaluma yake ya dini yaani upadri unaweza kumdhaba kibao shavu la kushoto na majibu yake yakawa hallelujah akageuza shavu la kulia umalizie hasira zako kisha mkaendelea na stori lakini hili la mapinduzi haramu na mtu ambae dk slaa alijipatia umarufu jinsi alivyokuwa akimuelezea kiasi gani lowasa alivyoneemeka na ufisadi si rahisi dk slaa kuvumilia Nasema mapinduzi kwa sababu hivi tunavyozungumza lowasa ni mtu mwenye maamuzi ya mwisho kichama hakuna anaemjua slaa tena. Njia moja ya kutubu kwa dk slaa madhambi yake ni kujiweka mbali kabisa na chadema pamoja na ukawa kwa sababu akishiriki shughuli yeyote ile chini ya uongozi wa lowasa hapana shaka dk slaa ni fisadi na mnafiki mkubwa atakuwa muovu zaidi ya lowasa. Lowasa anasema mchakato wa ccm haukumtendea haki na mwenye kiti kaja na kikaratasi chenye majina matano lake halikukuwemo kwa hivyo sio dekrasia sasa hao ukawa wangekuja angalau na kikaratasi chenye orodha ya majina mawili kabla ya kulipitisha jina la lowasa na kumfanya kuwa mgombea pekee sifikirii kama wanachadema na ukawa wametendewa haki.

Anonymous said...

Kinachomfanya Lowasa kushupalia kuwa rais ni kitu gani hasa? hii inashangaza sana ni nini kinamfanya ashupalie urais? au amepata wehu? mpaka kuhonga mabilioni tangia akiwa ccm eti anapendwa anapendwa na wenye pesa wenzie,kama yeye alionewa ccm mbona nae kamuonea Slaa, agekubali kuwa chadema kuongeza nguvu sio kusema nipewe urais, kutufanya waTanzania mazuzu asemacho mwenye pesa ndio sawa

Anonymous said...

Watu wenye Ubinafsi tu kama wenye maoni hapo juu ndiyo wanaoweza kutoa uongo ambao hauna Udhibitisho. Nawaona kama wadudu fulani wa ccm. Mtazikwa na ccm.

Anonymous said...

Ukweli siku zote unauma unapozungumzwa hasa kwa sisi wa afrka mtu akikwambia ukweli hata kama analengo la kukusaidia unaona kakutukana lakini hiyo ndio habari yenyewe Dr Slaa kamkimbia fisadi chadema sasa wewe jifariji kwa kuamini huo ni uwongo .

Anonymous said...

wewe mwandishi are you sure??

Anonymous said...

Lawasa ni MTU mwema hapendi ubinafsi, ameguswa kuwabariki viongozi wenzake kwa kuwagawia sehemu ya utjiri wake, mwacheni kumuonea wivu. Vigerege jamani akinamama, wababa mpigieni makofi lowasa jamani