Advertisements

Wednesday, July 1, 2015

Muda wa Jakaya Ndio Umeisha, Babu Seya Ndio Basi Tena?


Wanamuziki Nguza Viking na Papii Kocha wanaotumikia kifungo cha maisha jela, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasamehe kwa makosa waliyofanya.
Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi hilo kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Nguza maarufu Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete.

TAARIFA HII NI YA TEREHE 21/JUNI/2014. Mhe. Rais anamaliza muda na juzi alikuwa kule magereza akitunuku nishani. Alisema akisamehe baada ya muda wanaorudi kifungoni ni zaidi ya aliowasamehe.

No comments: