Advertisements

Tuesday, July 28, 2015

KAULI NANE ZA EDWARD LOWASSA WAKATI ANAJIUNGA NA CHADEMA LEO HIZI HAPA

 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.Picha na Ahmad Michuzi


Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), leo Jijini Dar na hizi ndizo kauli alizozitoa wakati wa hotuba yake

Lowassa: Namshukuru mke wangu Regina, wanangu na wanafamilia katika kipindi hiki kigumu kilichojitokeza.

Lowassa: Nawashukuru wanaCCM waliojitokeza kuniunga mkono wakati nikitafuta wadhamini.

Lowassa: Kilichotokea Dodoma, ni kupora madarakani ya kamati kuu, waswahili wanasema kubaka madaraka.


Lowassa: Chuki na roho mbaya zilitawala licha ya mimi kuwa mgombea mwenye ushawishi na anayekubali zaidi kuliko wote.

Lowassa:Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kudanganya nafsi yangu na Watanzania kuwa bado nina imani na CCM.

Lowassa: Sijakurupuka kwa uamuzi huu, nawaomba watanzania wajiunge na UKAWA katika Safari ya Matumaini.

Lowassa: Wanaoogopa kisasi wamefanya madhambi gani? Waulizeni..mimi ni Mkristo,sina kisasi..waende wakatubu kwa Mungu wao.

Lowassa: CCM Si baba yangu wala Mama yangu. Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM.

10 comments:

Mtanzania, Washington, D.C. said...

Acha unafiki Lowasa kwani CCM has made you who YOU ARE.! I.I.e. Educated by CCM. made RICH by CCM, made FAMOUS by CCM, etc. etc. and to that end CCM has been your FATHER and MOTHER in your POLITICAL LIFE. Unasema kuwa wewe ni MKIRISTO, kumbuka one of the TEN COMMANDMENTS inasema "WAHESHIMU BABA NA MAMA ILI UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI'. You need to REPENT Mr. Lowasa, GREED FOR POWER is your biggest SIN.

Anonymous said...

Desperation and selfishness at its highest!

Anonymous said...

"Sitaondoka CCM kamwe, bali asiyenitaka ndio aondoke" - E.Lowasa

Anonymous said...

Politics is a dirty game guys, I dont buy your blames to Mr Lowassa! As a politician he has to play that game. That is a challenge to those who think it is only ccm in Tanzania. Let us try to think outside the box!! If you think Dodoma was fare just wait the anger of Tanzanians with ccm on October 25.

Anonymous said...

NDIYO AMEAMUA KUONDOKA YEYE KUNA KOSA GANI? AMEELEZA UKWELI KUWA HAWEZI KUKAA NA WATU WENYE CHUKI NDANI YA CHAMA....HIVYO KAAMUA AONDOKE YEYE. ACHENI PROPAGANDA ZENU ZA CCM HAPA WASHINGTON....RAIS NA MWENYEKITI WENU WA CCM ANA KESI YA KUJIBU KUHUSU RICHMOND KWA SABABU YEYE NDIYE ALIYEAMURU RICHMOND IPEWE TENDER NA ISIFUTWE.

Anonymous said...

Mimi binafsi nampongeza, na niko tayari kufanya nae kampeni pande zote za Tanzania, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Ukawa. Cha msingi ni kuweka Human Resources pande zote kuhakikisha ushindi, waangalie mpango mzima aliotumia Obama kuhamasisha vijana kufanya Changes we Can believe in.....Please CHADEMA njooni vyuo vikuu mchukue hizo resources. We are ready.

Unknown said...

No l see it differently. Lowassa is strong determined. Lowasa anania anatetea nia na anamsimamo wa kudhamini wananchi Tanzanian at all level. He has been strong and will continue to be strong. Waliomdhamini wataendelea kumdhamini Lowasa siyo chama.
CCM is bullying. Byly is violence has to stop. Nyie mnaosikiliza CCM mnaunga violence ina maana kwamba mnatafuta ugomvi na wananchi.
People want Peace na ukweli. Acheni roho mbaya.

Anonymous said...

HIYO NDIO INAITWA SIASA MCHEZO. KWANI MWALIMU NYERERE ALIKOSEA TUSIDANGANYANE . CCM NI WABOVU ALIKOTUFIKISHA ALIYEKO MARAKANI NDIO HAPO!! Tusiwe na hasira nami nimeshaacha uCCM!!

Anonymous said...

Maamuzi magumu hata kubaki CCM ni maamuzi magumu.

Anonymous said...

You are wrong Vicky Rose and all others on LOWASA bandwagon! What has he done to the country during his tenure as a MP? If he was such a determined strong leader as you proclaim, why then he failed to clarify about his deep involvement in the Richmond scandal? Does holding a higher office (Presidency), make him a more effective leader than being a Monduli MP? All these fantasies, you the diehard fans have, is down-right garbage, because you thoroughly know deep-down in your hearts, that, Lowasa is power hungry; greed and only greed is the motive behind his overnight LOVE AFFAIR WITH UKAWA, wow!ROMANCE OF CONVENIENCE! Should he win, he will be the first VERY RICH candidate in the history of our country, to take over the Presidency. To all you misled followers, ask for yourselves; where? and how? did this fellow get all the wealth? Did he care about you when he was accumulating all that wealth? Did you or your families get a piece of that pie? Would you expect him to care for you, the poor, once he becomes the President? OOH ya? he will tell us the tricks of getting wealthy! Unfortunately, the majority of our citizens are ill-advised, and psychologically manipulated into believing that Lowasa and Ukawa are the messiah. It is quite the opposite, these folks intent is not to advance our nation economically, but to bestow power and prestige to themselves. Prove me wrong, what are the job track records of Slaa, Lipumba, Mbowe, Mbatia, Makani, and all other Ukawa cheerleaders? Beside their chart-topping theme song "CCM must Go...", what else have they done to the nation, all these years? Let us spare our country from disaster, Tanzania is not a laboratory, henceforth, we should not allow UKAWA to pursue their experiments. MUNGU IBARIKI TANZANIA.