Advertisements

Saturday, May 23, 2015

ZARI ATESWA NA PICHA YA KATUNZI.


Mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari’.

MUSA MATEJA
MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi.

Mtu wa karibu na Zari amefunguka kuwa Zari alijisikia vibaya sana baada ya kuona picha hiyo na kukasirika hivyo kuanza kuwasaka watu walioivujisha kwani walikuwa na nia mbaya ya kumgombanisha lakini wamechemka.
“Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo.
Supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wakeZarinah Hassan ‘Zari’.

Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
“Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.”
ZARI, PEDESHEE KATUNZI LAIVU!
Issa Mnally
KABAAANG! Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.
Credit:GPL

1 comment:

Anonymous said...

nilidhania zakuzua hizi story but sasaa nawasifu sana diamond,zarinah na wema sepetu na sasa tunawaona wengine wengi mastar wanafuata nyayo za hawa kina diamond,za kuuza sura zao kwenye magazeti.hizi story kama za shingongo zakutunga matukio mtakuja kusikia zari mimba imetoka ameachana na diamond etc wapo kibiashara hawa na kutuzunga sisi.

biashara ya magazeti naijui sana; big up guys;diamond,zari and wema .