Advertisements

Sunday, May 24, 2015

GWAJIMA, FLORA MBASHA WAIBUKIA MKUTANO WA CHADEMA KAWE, NI ULE WA KUZINDUA KITABU CHA MBUNGE HALIMA MDEE

Msanii wa nyimbo za Injili Flora Mbasha, (mwenye nguo nyeusi), akiongoza mashambulizi jukwani

MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, na mwibaji nguli wa muziki wa Injili Flora Mbasha, leo hii alasiri Mei 24, wameibukia kwenye mkutano wa hadhara wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Wakati Gwajima alihutubia, Mbasha alitumbuiza kwenye mkutano huo uliokuwa wa kuzindua kitabu cha Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA), Flora Mbasha chenye kichwa cha habari "Utekelezaji wa ahadi za mbunge 2011-2015".

Mgeni rasmi kwenye mkutano huo alikuwa ni mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Freeman Mbowe
Umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa hadaharab wa CHADEMA pale Kawe, vwanjavya Tanganyika Packers
Wafuasi wa CHADEMA wakisikiliza hotuba ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe
Mbowe, Mdee na Mnyika wakizindua kitabu hicho
Gwajima akiwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA
Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano huo
Mchungaji Gwajima akiongozwa na Halima Mdee kwenye jukwaa kuu
Mbunge wa Kawe akiongozana na Mchungaji Gwajima
Mchungaji Josephat Gwajima, akihutubia mkutano wa CHADEMA leo Jumapili Mei 24, 2015 pale Kawe Tanganyika Packers
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog

2 comments:

Anonymous said...

Where is the separation of church and state? This is a serious violation of our constitution!

Anonymous said...

seperation of church and state iko huko kwenu marekani si tanzania ebooo unajidai ung'a ng'a hapa.

wana chadema oyaaaaaaaaaaaaa dole tupu.