Advertisements

Wednesday, April 22, 2015

BAADA YA KUSAMBAA KWA PICHA ZA MWANASHERIA AKIFANANISHWA NA JAMBAZI HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

Mwanasheria wa serikali mara baada ya kumvisha pete mchumba wake(hii ndio moja ya picha inayo sambazwa katika mitandao ya kijamii)

Kutokana na kusambaa kwa picha katika mitandao ya kijamii zinazoonyesha vijana wanaosadikika kuwa ni majambazi waliokamatwa na jeshi la polisi siku ya jana, kijana aliyezungushiwa duara ambaye anaonekana katika picha akiwa na wenzake, anafananishwa na kijana anayeonekana  akiwa na mwenziwake katika shughuli ya kumvalisha pete ya uchumba mwenzi huyo, ambapo watu wengi wamekuwa wakipotosha jamii kwa kuweka picha zisizozake ambazo picha hizo zinafananishwa naye, picha hizo ni za mtumishi wa umma katika mahakama( Mwanasheria  wa serikali). Katika kipindi cha leo tena cha Clouds Fm mwanasheria huyo amekanusha kuwa yeye sio yule jambazi aliyekamatwa bali ni raia mwema na anaendelea kulitumikia taifa kama kawaida wakati majambazi hao wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Aliyezungushiwa duara jeusi ni mmoja wa majambazi yaliyokamatwa hapo jana(huyu ndiye anayefananishwa na mwanasheria huyo)

"Hapo jana mara baada ya tukio hilo kutokea la kuwakamata majambazi hao nilipigiwa simu na watu mbalimbali wa karibu waliokuwa wakitaka kunieleza kusambaa kwa picha zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii nikifananishwa na jambazi na hivyo kutokana na mimi nilikuwa katikati ya kazi sikuweza kutambua mapema kitu kilichokuwa kikiendelea mara baada ya muda wa kazi kupita ndipo nilipoona picha zangu zinazofananishwa na huyo jambazi zikiwa zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii" alisema mwanasheria huyo.

No comments: