Advertisements

Friday, January 23, 2015

Haya ni maneno ya Wema Sepetu kuhusu inshu ya kumdai Diamond

Ukubwa wa stori hii ambayo jana aliizungumzia Martin Kadinda kama Meneja wa Wema Sepetu imefanya millardayo.com kutaka kuujua undani zaidi kutoka kwa Wema mwenyewe.
Kwenye exclusive Interview,Wema amesema>>’Taarifa hii imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter,anaiendesha mtu wangu wa blog Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko’
‘Nilishasema ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena,nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila kitu ili kuepuka haya maneno’
‘Hakuna kitu ambacho namdai Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki Diamond labda kama kungekua kuna kitu chochote,yaani labda kungekua na ukweli wa kitu chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda polisi,sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana’‘Sijawahi kujiunga Vikoba maana sivijui,nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui hawa watu wa vikoba wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na kutengeneza hii kitu kwamba vikoba wanaweza kukopa hadi Milioni kumi kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10′


No comments: