Advertisements

Sunday, December 21, 2014

BIBI HUYU AUA MJUKUU WAKE WA MIAKA 6 KWA KUMTUPA DIRISHANI WAKATI BASI LIKIWA KATIKA MWENDO KASI HUKO SINGIDA

Bi Lawaridi sadi (46)akiwa kituo cha polisi mkoani singida kwa kosa la kutupa mtoto kwenye basi basi ililolilikuwa likielekea mkoani kigoma

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na mtoto wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika kwa jina la Lawaridi Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na basi namba T 981 ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea Dar-es-salaam na kuelekea Kigoma.

Amesema alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya tarehe 18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshack dirisani huku basi likiwa katika mwendo kasi.

Tayari jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mwanamke huyo.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida Dkt Adamu Hussen amesema alimpoke mtoto akiwa katika hali mbaya akiwa hapumui vizuri na damu ilikuwa ikimtoka masikioni na baada ya kumpatia matibabu alilazwa na siku ya pili alifariki dunia kutokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa.
Akieleza jinsi alivyo mtupa mjukuu waka,Lawaridi Saidi ambaye ni mkazi wa K ongowe jijini Dar es salaam amesema baada ya kuamka akiwa katika hali ya usingizi alijikuta akimchukua mjukuu wake Mayasa na kumtupa dirishani na hatimaye abiria wakaanza kumpiga na kuamuru basi lisimame na kumchukua mtoto huyo.

1 comment:

Anonymous said...

Jamani, tafadhali mpelekeni hosptali akapimwe akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hivyo. Huyo mama ni mgonjwa msimpige.