Advertisements

Friday, November 28, 2014

ZITO ALIPULIWA NA RAFIKI YAKE KIPENZI, LUSINDE PESA ZA ESCROW NAE YUMO

Hii ndiyo barua iliyoandikwa na zito kwa ajili ya kukopa fedha hizo za Escrow kumpeleka mama yake india kutibiwa. Barua hii iliyo na vithibitisho kadhaa pamoja na kopi ya leseni ya aliyetumwa iliwasilishwa na Mbunge Lusinde Bungeni na kusomwa kisha kuikabidhi meza kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Lusinde akichangia wakati wa mjadala huo ukiendelea Bungeni jana jioni huku akionyesha barua hiyo inayomhusisha Zito katika kashfa hiyo.
Lusinde akiendelea kuchangia huku akiwavunja mbavu wabunge kwa vijembe vyake.
Mbunge Kafulila, akichangia kujaribu kuthibitisha ukweli wa sakata hilo.
Kafulila akiendelea kumwaga nondo.
Mbunge, Joshua Nassari, akisimama kuomba mwongozo, jambo lililomfanya mwenyekiti wa kikao hicho, Zungu kuingilia kati na kupiga marufuku wabunge kuomba mwongozo wakati mmoja wao akiendelea kuchangia, kutokana na kuchelewesha muda.
Sehemu ya wabunge waliohudhuria kikao hicho cha jana jioni. Sfiani Mafoto

4 comments:

Anonymous said...

Hiyo barua ni feki, kwani kama ni mkopo wa millioni 6 kukopa kwa mtu binafsi huwezi kueleza sababu za kuomba mkopo. "ETI MKOPO KWA AJILI YA KUMPELEKA MAMA HOSPITALI" asiyejua ni feki ana matatizo ya kufikiri, kwanza barua imetaka kusema "my mother" akafuta "my" badala yake akasema 'his, hao ni wahuni walioandika hiyo barua.

Anonymous said...

Yaani hawa wabunge ni kama watoto kwakweli,they acting so childish

Anonymous said...

Upuuzi mtupu msitake kutupotosha eti tukose kukomaa na wezi. Zito komaa nao hao asante sana kwa kujitoa mhanga kwa taifa. Mungu akutunze!!!!!!

Anonymous said...

Na hii barua kama ni feki huyu Lusinde achukuliwe hatua. This man has no respect for parliament house or his fellow MP's. Hawa watu wanafikaje bungeni