Advertisements

Monday, July 21, 2014

KAHABA WA TANZANIA ASIMULIA JINSI ALIVYOUSAMBAZA UKIMWI KWA MAELFU YA WANAUME

MWANAMKE
mmoja wa Kitanzania aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika miji 
mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam
na mingine ya Namibia, ameibuka na kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya 
kusambaza Ukimwi kwa wanaume wakware.
Licha
ya kukiri kufanya hivyo, akisema kwa siku alipanga hadi wanaume 
watano,tena bila ya kutumia kinga akisema alidhamiria kuusambaza ugonjwa
huo hatari alioambukizwa akiwa katika shughuli za ukahaba.
Alijigundua
ameathirika mwaka 2006. Hata hivyo, katika maelezo yake ameelezea 
kuijutia dhamira yake hiyo, akisema alisambaza kutokana na hasira 
aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume aliyemwambukiza.


“Nilimchukia
sana kila mwanamume, yeyote aliyejiita mwanamume…nilishindwa tu 
kuwawinda na kuwaua, lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia silaha yoyote kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua
mwangu nilijisemea kamwe sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote 
anayekuja kwangu nammaliza. Kwa namna walivyoniambukiza lazima niwaambukize’. "Sijui nimewaambukiza wanaume wangapi, lakini ni maelfu,” alisema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria hivi karibuni.

5 comments:

Anonymous said...

Kwaiyo anaendeleza kusambaza uko nigeria je munachukuwa atuwa gani na mshamjuwa?

Anonymous said...

Now she is okay since she gave her life to Christ

Anonymous said...

Allijuaje kama hao ambao anasema aliwaambukiza ukimwi hawakuwa na ukimwi kabla ya kukutana nae? Labda na wao walikuwa wameathirika ndio maana hawakutumia kinga.

Anonymous said...

Mumuombee kwa mungu kwakua ameshajutia .dhambi zake ndo mana amejisalimisha kanisani.

Anonymous said...

She gave her life to Christ. HahahaHh. How many more sins can Christ take?. Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.