Advertisements

Friday, July 18, 2014

BABA YA DIAMOND ALALAMIKA KUHUSU MWANAE


Stori: Erick Evarist na Gladness Mallya
Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akila ujana na mpenzi wake Wema Sepetu.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.

BOFYA HAPA
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”

MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.
Mama yake Diamond,Sanura Kassim ‘Sandra’ akilitesti gari alilokabiziwa na Mwanaye kama zawadi.

“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.

UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.

MATANUZI YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

Baba yake Diamond, Abdul Jumaa akitafakari jambo.

TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:

“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.

“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.

“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.

DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!

9 comments:

Anonymous said...

Mnaongea kwasababu hamjawahi kutelekezewa watoto na kuanza kuhangaika nao kama chizi. Don't talk before you know the inside story of the people. Wanaume wengi mnatuachia watoto wakipata maendeleo ndio unajijua kama ni baba ulikua wapi siku zote, Diamond hata akifa usiende kwenye mazishi. Ndivyo nnavyosema mimi kwa babangu na kwa baba wa mtoto wangu

Anonymous said...

Cha muhimu ni kumsamehe baba yake kama alimkosea. Km anaona yakuwa hawezi kumsamehe na amekuwa akisamehe wengine, basi ampe tu msaada km vile amabvyo anaweza msaidia mtu baki.

Wakati mwingine shida hutokea km mzazi wa kiume alimkataa mama na watoto, mama akahangaika mwenyewe ili wanae wapate mafanikio.baba anaponda raha,zina mwisho wake. Watoto hukumbuka yaliyopita na si wote husamehe na kujishusha.
Wazazi pia tuwe na upendo maana hujui ni motto yupi atakusaidia kesho.

Anonymous said...

Nyie Global Publishers msiyoyajua ya watu muyawachage hivyo hivyo. Kuna ugomvi mwingine hautatuliwi magazetini. Muacheni Diamond ni kijana mwenye busara anayejua alipotoka, kama hataki kumsaidia babake anasababu zake.Acheni kumchimba

Anonymous said...

Nyie Global Publishers msiyoyajua ya watu muyawachage hivyo hivyo. Kuna ugomvi mwingine hautatuliwi magazetini. Muacheni Diamond ni kijana mwenye busara anayejua alipotoka, kama hataki kumsaidia babake anasababu zake.Acheni kumchimba

Anonymous said...

kwani diamond ndio mtoto pakee WA huyo baba? Mbona ana mtoto mwingine muimbaji yul e queen Darleen na hamumuandiki kwenye magazeti?????ache hizo!!!!mbona alipokuwa amemtoroka mama na huyo Diamond hakujitokeza kwenye magazeti kama aache njaaa huyo mzee.

Anonymous said...

Baba yake Diamond alikuwa Wapi?.Hayo ndiyo matokeo ya kutupa jongoo na mti wake. Muumba hatakubali laana yako. Laana hiyo ndiyo uipatayo kwa kuwatekeleza.Publishers inaona hamfanyi utafiti wa habari acheni rhizome.Mastaa wengi yamewakuta kama Diamond kmno, Shaw,Lebron,Jobs nk.

Anonymous said...

Wanaume wetu wengi wanajisahau. Hapa DMV wamejaa. Wanatupa watoto baadae eti wanajifanya ma BABA. hata mimi nisinge msamehee. Endelea DIAMOND. Mwangalie mama yako

Anonymous said...

jiulize kama wewe huwezi kumsamehe mwenzako je mungu akisema na yeye hakusamehe itaonaje/utajisikiaje?

tuwe na miyoyo mema ya kusameheyana hakuna aliyekamilika illah Allah kila mmoja wepo tuna kasoro zetu.

Anonymous said...

Mbona Wema alimtenda lakini amemrudia na kumsamehe. Hata baba Yake alimkosea na yeye ni binadamu. Msamehe baba yako na Ndugu zako. Hata sisi wanadamu tunaomba Mungu atusamehe sasa inakuwaje huwezi kumsamehe baba yako.