Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

HANDAKI LA AJABU LAONEKANA ENEO LA KITANZINI IRINGA.. SHUHUDIA


Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo
mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa nyumba ambayo handaki hilo limeonekana
Handaki lenyewe muonekano wa sehemu ya kuingilia
Mkuu wa Wilaya kushoto aipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazio wa kampuni ya maji Iringa
 
 
Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi. Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo. Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo. 
Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani. 
Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa. mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo. nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo? Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote. PICHA NA FRANCIS GODWIN

No comments: